Guardiola: Man United imepata Kocha Mzuri kwa Miaka Mingi

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema kua klabu ya Manchester United imepata kocha mzuri ambaye watakua nae kwa muda mrefu ambaye ni kocha raia wa Uholanzi Erik Ten Hag.

Pep Guardiola amemsifu kocha Ten Hag leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa fainali ya kombe la FA Cup kati ya Manchester United na Manchester City, Ndio wakati kocha huyo alipoamua kumpa maua kocha mwenzake Erik Ten Hag kuelekea mtanange wao.Guardiola“Siwezi kusema sisi ni marafiki, Kwakua hatupo karibu sana lakini nafikiri Manchester United wamepata kocha wa daraja la juu kwa miaka mingi”Aliyazungumza hayo kocha huyo bora wa msimu nchini Uingereza akifanikiwa kuipatia klabu yake ya City taji la tatu mfululizo la ligi kuu ya Uingereza.

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag anapokea sifa kwa watu tofauti tofauti kutokana na kazi kubwa ambayo ameifanya ndani ya klabu hiyo ndani ya msimu wake wa kwanza ndani ya United, kwani mpaka sasa amefanikiwa kuirudisha klabu hiyo kwenye ligi ya mabingwa na kubeba taji moja la Carabao na kesho anacheza fainali ya kombe la FA.GuardiolaKocha Guardiola pamoja na wadau wengine wanaamini Erik Ten Hag anaweza kuirudisha Manchester United kwenye zama zake za mafanikio, Kwani mpaka sasa kocha huyo ameonesha mwanga ndani ya klabu hiyo tofauti na makocha wengine ambao wamepita ndani ya klabu hiyo miaka kadhaa nyuma.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.