Gueye na Garner Kuwakabili Liverpool

Kocha wa klabu ya Everton Frank Lampard amethibitisha kuwa wachezaji wake wawili wpya Gueye na Garner aliwaosajiri kabla ya dirisha kufungwa usiku wa jana wako tayari kuwakabili mahasimu wao Liverpool.

Gueye na Garner wote wamesajiriwa kwenye nyakati za mwaisho wa dirisha la usajiri, baada ya Frank lampard kutaka kuimarisha safu yake ya kiungo, kwani Everton walikuwa wanafanya mazngumzo na Gueye tokea dirisha kufunguliwa, wakati Garnier akijiunga na klabu hiyo kutokea man Utd kwa ada ya uhamisho ya  £9m.

Lampard alinukuliwa akisema: “Gueye ni mchezaji kwa sasa, bila shaka, klabu inamjua vizuri na yeye anajua vizuri klabu. kwenye upande wa ubora, yeye anacheza kiungo cha chini, namba sita au nane ambayo amekuwa akicheza PSG sana.

“Ananipa machaguzi mazuri na uzoefu mzuri. Yeye ni mchezaji wa tofauti kwa jinsi tulivyompata, hivyo kiukweli, kiukweli tunashukuru kuwa nae. James Garner, kwenye mikakati ya kunyumbulika ni mzuri, bado kijana ana nguvu nyingi na ubora mkubwa atajiboresha na tutamporesha.”

Pia Lampard aliongezea kuwa Gueye na Garnier, kwamba wanaweza kuwepo kwenye kikosi cha kesho kwenye dabi ya Merseyside, japo hakuweka wazi kama wataanza au wataokea benchi.

 

 

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.