Guirassy Kuondoka Borussia Dortmund Mwisho wa Msimu

Mshambuliaji hatari wa Borussia Dortmund, Serhou Guirassy, anaripotiwa kuwa tayari ameweka wazi nia yake ya kuondoka klabuni mwishoni mwa msimu. Licha ya kuwa na mkataba hadi 2028, nyota huyo wa Guinea anataka changamoto mpya, na tayari klabu kadhaa zimeanza kuonyesha nia ya kumsajili.

Guirassy Kuondoka Borussia Dortmund Mwisho wa Msimu

Inaelezwa kuwa Guirassy ana kipengele cha kuachiliwa kwa euro milioni 35 kitakachoanza kufanya kazi majira ya joto, lakini kwa masharti maalum, kikilenga vilabu vikubwa kama Real Madrid, FC Barcelona, Manchester United, Manchester City, Arsenal, Chelsea na Liverpool. Hii inaacha mustakabali wake wazi kwa dili kubwa.

Vilabu kama AC Milan na Fenerbahçe vinaonekana kuwa mstari wa mbele, huku pia timu za Premier League na Saudi Arabia zikitajwa kuvutiwa naye. Ingawa Saudi Arabia ilionekana kuwa chaguo la kifedha, sasa inaelezwa kuwa si kipaumbele chake kikuu.

Guirassy Kuondoka Borussia Dortmund Mwisho wa Msimu

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa upande wa Dortmund, hili ni pigo kubwa kwani Guirassy ndiye kinara wa mabao. Hivyo, uongozi wa klabu tayari unaangalia mbadala wake, huku majina mawili yakitajwa zaidi, Nicolo Tresoldi na Fisnik Asllani.

Guirassy Kuondoka Borussia Dortmund Mwisho wa Msimu

Tresoldi anaonekana kuwa chaguo la bei nafuu bei yake ikiwa ni euro milioni 25–30 na tayari ameonyesha kiwango bora, wakati Asllani naye ana kipengele cha euro milioni 30 lakini anakabiliwa na ushindani kutoka FC Barcelona, ambao nao wanamfuatilia kwa karibu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.