Washambuliaji watatu jana wamevunja rekodi iliyodumu kwa muda wa miaka 28 baada ya kufunga Hat-trick katika michezo ya jana ambao ni Earling Haaland wa Man City Evan Ferguson wa Brighton na Heung ming Son wa Tottenham.

Earling Haaland na wenzake jana walifanikiwa kuvunja rekodi ya kina Alan Shearer, Robbie Fowler pamoja na Tony Yeboah ambao walifunga mabao matatu kwa siku moja katika siku moja ya michezo ya ligi kuu ya Uingereza.haalandBaada ya Alan Shearer,Robbie Fowler,na Tony Yeboah kufunga mabao matatu kwa siku moja katika michezo ya ligi kuu ya Uingereza haikuwahi kutokea tena mpaka jana ilipotokea tena kwa washambuliaji Haaland, Ferguson, pamoja na Heung Ming Son hapo jana.

Mshambuliaji Halaand yeye alifanikiwa kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao matano kwa moja walioupata klabu ya Manchester City dhidi ya klabu ya Fulham hapo jana na kuiwezesha timu yake kupata alama tatu.haalandMshambuliaji Heung Ming Son nae alifunga mabao matatu kwa moja katika ushindi waliopata Tottenham jana, Huku Evan Ferguson akifunga mabao matatu yaliyoipa klabu yake ya Brighton ushindi wa mabao matatu kwa moja mbele ya Newcastle.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa