Hazard Hati Hati Kutocheza Mpira Tena.


 

Daktari ameonya kwamba kiungo fundi wa Real Madrid, Eden Hazard anaweza asicheze mpira kamwe iwapo atafanyiwa upasuaji mwingine wa kifundo cha mguu (ankle).

Mbelgiji huyo amekuwa akisumbuliwa na majeraha tangu ajiunge na Real Madrid akitokea Chelsea kwa mkataba wenye thamani ya hadi pauni milioni 130 nyuma mwaka 2019.

Amewekwa pembeni na shida nyingine ya kifundo cha mguu kwa sasa na inaeleweka anataka operesheni nyingine.

Lakini Dkt Jose Gonzalez, ambaye anafanya kazi kwa wapinzani wa Real, Atletico Madrid, alionya kuwa operesheni ya tatu ya kifundo cha mguu inaweza kumaliza kazi ya Hazard (kucheza soka).

 

Alimwambia Ondacero: ‘Hazard lazima afanye mazoezi na timu hadi vikao 10 vya mazoezi.

Kwa uzoefu wangu ni ngumu kwake kurudi kucheza kwenye kiwango chake na Real Madrid msimu huu.

“Ikiwa mchezaji anarudi baada ya kuumia kwa muda mrefu bila kupata mazoezi magumu, jambo la kawaida kuina kuwa mchezaji ameumia tena.

Ana wasiwasi, anataka kuonyesha kuwa ana thamani na anataka kutoa 100% na hayupo kwa hiyo.

‘Operesheni ya tatu kwenye kifundo cha mguu cha Eden Hazard ni hatari sana, kuna uwezekano wa kuwa mchezaji hangecheza mpira tena.’

Hazard ameripotiwa kusafiri kwenda London kutafuta maoni ya pili juu ya jeraha hilo.

Alirudi tu hivi karibuni katika ushindi wa Jumamosi wa 2-1 dhidi ya Elche na Zinedine Zidane alisema “hawezi kuelezea” kwanini mchezaji huyo wa miaka 30 alipata shida nyingine.

Real ingependa kuahirisha upasuaji lakini Ubelgiji ina hamu ya Hazard kushughulikiwa na shida haraka iwezekanavyo ili aweze kurudi katika hali ya usawa kwa wakati uliohirishwa wa Euro 2020 msimu huu wa joto.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

CHEZA HAPA

7 Komentara

    Hii hatari kwa hazard

    Jibu

    Kijana pole Sana

    Jibu

    Duuh pole yake

    Jibu

    Habari mbaya hi

    Jibu

    Eeh makubwa

    Jibu

    Polee yake

    Jibu

    Jamani apone tu bado tunahitaji uwepo wake

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.