Neymar Jr ataungana tena na Lionel Messi huko Camp Nou hii ni kwa mujibu wa wakala wa zamani wa Kibrazil na skauti wa zamani wa Barcelona Andre Cury.

Cury alitumia muda wa miaka 10 kufanya kazi na Barcelona akiwa kama wakala wao nchini Brazil na alifanya kazi kubwa katika uhamisho wa Neymar kutua Barcelona.
Baada ya kushirikiana na Messi msimu ambao Barca ilishinda LaLiga 2014-15 na 2015-16na Copa del Rey tatu Neymar aliondoka Barcelona na kwenda Paris Saint-Germain mwaka 2017 lakini Cury amesema wawili hao wanaweza kuungana tena.
Messi amekuwa akihusishwa na kuihama Barcelona, na vilabu vilivyokuwa vinahushishwa ni PSG na Manchester City lakini Cury anasema anahisi wawili hao wanaweza kuwa pamoja tena huko Catalan.
“Miaka miwili iliyopita Neymar aliniomba anataka kurejea Barcelona tulijaribu na tulikuwa karibu kukamilisha mpango huo.cury aliiambia El Litoral.
“Mtu pekee anayeweza kuwaunganisha tena wachezaji aho ni rais mpya wa Barcelona Joan Laporta, Messi hataki kuondoka tena Barcelona ameamua maisha yake na historia yake iwe ni Barcelona.
“Neymar atacheza tena na Messi lakini itakuwa huko Barcelona.
Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.



Dorophina
Hii itakuwa poa miamba hao wawili wakikutana
Adelta
Itakuwa bonge la mechi
Lydia Emmanuel Magoti
Itakuwa bab kubwa hii
Caroline
Hii si ya kukosa
Sarah
Itakuwa mechi kali
Hopemwaikuka
Itakua njema
Neema juma
Kutanoga uwanjanii
warda
Itakuwa safi sana