Howe: Hakuna Haja ya Kulalamika.

Kocha mkuu wa klabu ya Newcastle United Eddie Howe amesema kuwa haoni haja ya kulalamika kutokana na kile kitendo kilitokea katika mechi yao iliyopita dhidi ya Liverpool ambapo walikuwa wageni wa mchezo huo.

Howe: Hakuna Haja ya Kulalamika.

Kauli hiyo inatokana na kitendo cha refa wa mchezo  huo kuongeza dakika 8 kitu ambacho
kilifanya wafungwe bao ambalo  liliifanya  Liverpool aondoke na alama tatu za muhimu. ambapo bao hilo la kuipa Majogoo alama tatu  lilifungwa na Fabio Carvalho.

Baada ya kupoteza mchezo huo kocha wa timu hiyo Howe alisema kuwa haoni umuhimu wa kufanya hivyo kwani hata wakilalamika hawaoni faida yoyote kwenye kulalamika kwani watawekeza nguvu kwenye kitu chanya na chenye thamani zaidi, na hiyo itakuwa kwa wachezaji wangu kila wakati.

Howe: Hakuna Haja ya Kulalamika.

Newcastle ambayo msimu uliopita imenunuliwa na Saudi Arabia’s Public Investment Fund na washirika wengine wameifanya timu hiyo kunusurika kushuka daraja na kumalizia msimu wakiwa nafasi nzuri, Lakini pia wamefanya usajili mzuri msimu huu akiwemo nyota wa zamani wa Real Sociedad na timu ya Taifa ya Uswis Alexander Isak ambaye mechi yake ya kwanza tu dhidi ya Liverpool alitupia bao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.