Christian Eriksen amewaonya wachezaji wenzake wa Manchester United kwamba, lazima waonyeshe uwezo mkubwa zaidi dhidi ya Arsenal Jumapili baada ya ushindi wa jana dhidi ya Leicester City.

Kikosi kipya cha Erik ten Hag kilitawala dakika 45 za kipindi cha kwanza kwenye uwanja wa King Power, lakini bao la Jadon Sancho lilichukuliwa kwa ustadi kuonyesha ubora wao.
Kikosi cha Brendan Rodgers kinachotatizika kiliimarika baada ya mapumziko, na United walikuwa na deni kwa kipa David de Gea kwa kulinda bao la kuongoza huku Mashetani Wekundu wakiendelea kuandikisha ushindi wao wa tatu mfululizo.
United itawakaribisha vinara Arsenal katika uwanja wa Old Trafford wikendi hii, katika hali ambayo inaenda sambamba na mafanikio yao ya hivi karibuni na Eriksen anajua kuwa Arsenal hawataruhusu Utd kucheza kwa uhuru.

Eriksen: “Ndio, nadhani tangu mwanzo tulikuwa, tulikuwa na mambo mengi ambayo tulihitaji kubadili na tumefanya hivyo kwa kushinda.
Eriksen: “Haikuwa nzuri kwa dakika 90 lakini tumeshinda mara tatu. Nadhani kwa sasa tunashinda 1-0 na kuzuia tusifungwe”.
Eriksen: ”Ni wazi tunataka kufanya vizuri zaidi, lakini ni mwanzo mzuri, tunaweza kuchukua kitu kutoka kwa hili na pointi tatu ndizo muhimu zaidi.

Eriksen; Nadhani tulipaswa [kuumaliza mchezo], ilikuwa sawa na Southampton. Tulifanya vizuri sana hadi tukafunga.
Eriksen: “Lazima tuendelee na kasi, tunapaswa kumaliza mchezo mapema, vinginevyo utakuwa mchezo mgumu hadi mwisho kama leo (Septemba 1, 2022).
Eriksen: ”Kuanzia sasa michezo inaendelea tu, Alhamisi hadi Jumapili, tunaonekana vizuri na kupata pointi.”