Mchezaji wa klabu ya Atletico Madrid raia wa Ureno Joao Felix ameingia kwenye rada za klabu ya Manchester United kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari.
Klabu ya Manchester United imepanga kuingia sokoni kwenye dirisha dogo mwezi Januari ili kukiboresha kikosi chake katika eneo la ushambuliaji, Kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag aliweka wazi kua lazima wingie sokoni dirisha hili ili kuboresha timu yao.
Mchezaji Joao Felix tangu ameanza kuhusishwa kuandoka ndani ya klabu ya Atletico Madrid na klabu ya Man United imekua ikinyemelea huduma yake kwa kiwango kikubwa, Ikimbukwe klabu hiyo imepanga zidi kutafuta mchezaji wa eneo la mbele na mchgezaji huyo anaweza kucheza maeneo mengi katika eneo la ushambuliaji.
Klabu ya Man United inatajwa kufanya mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo anayejulikana kama Jorge Mendes ili kuangalia uwezekano wa kumpata mchezaji huyo, Huku Felix nae akionesha anahitaji kuondoka ndani ya Atletico.
Klabu ya Manchester United inaelezwa kuongeza kasi ili kukamilisha dili la Joao Felix kwasababu wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka katika klabu ya Chelsea, Wakati huohuo United imemkosa Coady Gapko ambaye amejiunga na Liverpool kutoka klabu ya PSV Eindhoven.

