Klabu ya Manchester City inaelezwa haina mpango wa kumuuza mshambuliaji wake raia wa kimataifa wa Argentina Julian Alvarez ambaye anahitajika na vilabu kadhaa barani ulaya.
Vilabu kadhaa barani ulaya vimekua vikifukuzia saini ya Julian Alvarez moja ya vilabu hivo ni klabu ya Chelsea, Lakini Man City hawana mpango wa kumuachia mshambuliaji huyo chaguo la pili klabuni.Mshambuliaji huyo inaelezwa anataka dakika zaidi za kucheza ndani ya timu hiyo hivo malengo yake ni kupata timu ambayo itampa dakika zaidi, Huku klabu ya Manchester City yenyewe ikitaka kumbakiza klabuni hapo.
Klabu ya PSG inaelezwa kuwasiliana na wakala wa mshambuliaji huyo ili kuangalia uwezekano wa kumpata mchezaji huyo kuelekea msimu ujao, Lakini klabu ya City wametia ngumu kwa mchezaji huyo kutimka klabuni hapo.PSG, na Chelsea ndio vilabu ambavyo vinafatilia kwa karibu saini ya mshambuliaji Julian Alvarez, Hivo inasubiriwa maamuzi ya mwisho ya mshambuliaji huyo kama ataamua kuondoka ndani ya klabu hiyo basi vilabu vya Chelsea, na PSG ndio wana nafasi ya kumchukua mchezaji huyo.