Klabu ya Juventus imeanza mazungumzo na kiungo wa kati wa Borussia Dortmund, Axel Witsel kwaajili ya kumsajili katika dirisha la majira ya baridi kulingana na taarifa kutoka Sky Sports Germany.

Witsel, 32 anatakiwa na Juventus na mazungumzo baina ya klabu na wakala wa mchezaji yameanza, Usajili wa kiungo huyo hauta athiriwa na uuzaji wa wachezaji wengine.
Kulingana na taarifa nchini Ujerumani Borussia Dortmund wapo tayari kumuachia Witsel kuondoka ndani ya klabu hiyo na kuangalia mbadala wake mapema katika dirisha la usajili.
Bado hakujawana taarifa maalumu endapo Juventus wamepeleka ofa rasmi kwa Dortmund au ni tetesi kwasasa. Juve wamepanga kuwaachia Ramsey, Mc Kennie na Manuel Locatelli.
Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.


