Juventus Wamelaaniwa UEFA

Baada ya kutolewa kwenye Michuano ya Ulaya – UEFA kwa faida ya goli la ugenini dhidi ya Olympique Lyonnais. Kocha wa JuventusMaurizio Sarri anadhani timu yake imelaaniwa katika michuano hiyo.

Katika mchezo wa kwanza, Lyon waliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Juventus na hivyo kuifanya mechi yao ya marudiano kuwa ngumu zaidi. Juventus waliihitaji ushindi wa zaidi ya goli 2 ili kufuzu hatua ya robo fainali ya Michuano ya Ulaya – UEFA.

Juventus
Depay akifunga goli dhidi ya Juventus

Magoli mawili ya Cristiano Ronaldo hayakutosha kuivusha Juventus kwenda hatua ya robo fainali. Mshambuliaji Mephis Depay alikuwa wa kwanza kuzitingisha nyavu za Juventus na hivyo kuizamisha kabisa timu ya Juventus.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Sarri amesema ”  tumetolewa kwenye michuano ambayo tumeshinda michezo 6 kati ya 8 tuliyocheza, tumesuluhu 1 na kupoteza 1. Hii inamaanisha katika michezo 8 tumekusanya pointi 19″

Juventus
Cristiano Ronaldo baada ya kusawazisha goli kwa mkwaju wa penati.

“Kama kungekua na msimamo wa Michuano ya UEFA, tungekuwa wa kwanza au wa pili, lakini tumetoka. Ndio maana ninajisikia vibaya sana, inanifanya nielewe kwamba Juventus tumelaaniwa kwenye michuano hii.”

“Nisingekuwa na uchungu, ningetoka kwenye hii mechi nikiwa na uso wenye tabasamu kwa sababu nimewaona vijana wakicheza vizuri. Wamejitahidi kwa kila walichoweza kukitoa uwanjani kwa moyo wao wote mpaka mwisho wa mchezo, nimefurahi kwa hilo.”

Lyon na Juventus wote walipatiwa penati za kutatanisha, Ronaldo na Depay walitumia fursa hizo kufunga magoli. Sarri ameonekana kutofurahishwa na penati waliyopewa Lyon na kwamba kwake yeye haikuwa sahihi.

Juventus
Kocha wa Juventus – Maurizio Sarri

Sarri amesema ” Tulicheza vizuri katika mchezo ambao tulitokea nyuma ili kupata matokeo. Tulijikuta  tumefungwa kwa sababu ya penati ya kijinga. Kwa maoni yangu wasingepaswa hata kufika kwenye boksi kwa sababu ya madhambi aliyofanyiwa Gonzalo Higuain. Ile penati ni mjadala.”

“Refa hakuonesha uwezo wake katika nafasi kama ile. Kwa sisi kufungwa lile goli moja, kwetu ni kama tulifungwa magoli mawili. Tulikuwa vizuri kwasababu tulibadilisha matokeo lakini tulitumia nguvu kubwa sana”.

Juventus
Cristiano Ronaldo baada ya kufungwa na Lyon

“Tulipata nafasi mbili au tatu za kufunga magoli dakika za mwisho kwa vichwa vya Ronaldo, Higuain nadhani na Leonardo Bonucci, nadhani tulikuwa karibu kufuzu. Kama tunapaswa kulaumu, basi tunapaswa kujilaumu kwa mchezo wetu wa kipindi cha kwanza tulipokuwa Lyon. Katika viwango hivi, ni kitu unapaswa kulipia”.

Kwa ushindi huu wa Lyon, unaifanya Juventus kuendelea kusubiri kubeba kombe la UEFA tangu mwaka 1996.


Tiketi yako ya kwanza kamwe haiwezi kupoteza ukiwa na Meridianbet. Unarudishiwa 100% ya Tiketi yako ya kwanza.

Ingia Mchezoni

39 Komentara

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Asante kwa makala nzuri
    #meridianbettz

    Jibu

    Ni kweli juventus walijitaidi sana ila ndio hivyo tena bahati haikuwa kwao..!wasimame wajipange upya

    Jibu

    Sio laana ni bahati tu haikuwa upande wao

    Jibu

    Asante kwataharifa

    Jibu

    Asante kwa makala nzuri

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Kibibi kizee cha Turin inabid wajenge timu upya maana kila msimu wanaonekana wanaishia pale pale

    Jibu

    juve walifanya kila jitihada lakini hazikufanikiwa chochote

    Jibu

    Lyon walijihakikishia nafasi toka mwanzo alafu walikua na hali ya ushindi ingawaj juve walipigana pia

    Jibu

    Juve siolana ilandio mchezo walizidiwa kwaio wajipange sasa

    Jibu

    Asante kwa makala mzur

    Jibu

    Juventus imeweka nguvu nyingi kwenye Kombe hili lakini mara zote mambo yamekuwa magumu kwao. Inatakiwa kusajiri wachezaji watakaowezesha kufikia lengo hilo#meridianbettz

    Jibu

    Kila kitu kinaenda kwa riziki haikuwa riziki yao

    Jibu

    Akuna UEFA ngum sanaa

    Jibu

    Wajipange tu

    Jibu

    Walijitahidi sana juve lakini ndo ivyo haikuwa bahati yao

    Jibu

    Si laana ila bahat haikuwa upande wao

    Jibu

    Hapana sio laana bc tu wakati haujafika

    Jibu

    Juve wana wachezaji wazuri ila hawajitumi.

    Jibu

    Juve kwa msimu huu wamebologa labda wajipange mwakani

    Jibu

    Pambanen

    Jibu

    Kiukweli Lyon wamekuwa na bahati zaidi ya Juventus

    Jibu

    Nice update 👍

    Jibu

    Inapaswa watambue kwamba mpira Una mambo matatu na wahenga wanasema asiye kubali kushindwa sio mshindani.

    Jibu

    Kikubwa kujiweka sawa na kujipanga vzr kwenye msimu hujao

    Jibu

    Wajipange msimu ujao

    Jibu

    Asante kwataarifa

    Jibu

    Huyu mzee kweli anazeeka na kiburi

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Yawezekana ni kweli maana kila msimu wanatolewa mapema na ukiangalia Wana timu nzuri tu

    Jibu

    Wajipange upya

    Jibu

    Si bahati yao mana kutoshinda au kutolewa sio kwamba wamelaaniwa bado zamu yao mbona Liverpool walikaa miaka mingi bila kupata ubigwa sasa wanaushehekea ipo siku nao watavunja ukimnywa wao

    Jibu

    Juve wapo vizuri sana hila hawajitumi#meridianbettz

    Jibu

    Juve wapo vzr

    Jibu

    Duuuh wajipange tu watakua sawa

    Jibu

    Safi sana sarri umezungumza kijasir sana kama kocha na kuto kuwavunja moto wachezaj wako ingekua kama ndio kocha wa yangawalio mtimua basi nahisi ange watukana wachezaj au hata kuwakashfu kuwa walibeteka

    Jibu

    Hii ilimuuma sana CR7

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.