Leeds wamethibitisha kuwa Sam Allardyce hatakuwa kocha wao msimu ujao baada ya klabu hiyo kushuka daraja kwenye michuano hiyo.

Aliyekuwa mkufunzi wa Uingereza Allardyce mwenye miaka 68, alichukua mikoba ya Elland Road zikiwa zimesalia mechi nne kabla ya msimu wa Ligi Kuu kumalizika lakini hakuweza kuwabakiza ligi kuu.
Allardyce aliiambia tovuti ya klabu hiyo: “Imekuwa heshima kuisimamia Leeds United, klabu kubwa yenye mashabiki wa ajabu, ambao wanastahili kuwa kwenye Ligi kuu. Nimefurahia sana kufanya kazi na wafanyakazi na wachezaji katika klabu na ningependa kumshukuru Angus Kinnear kwa nafasi hiyo.”

Ningependa pia kuangazia kazi bora ya Karl Robinson na Robbie Keane ambao wamefanya kazi bila kuchoka katika wiki chache zilizopita. Kwa wakati huu wa maisha yangu sina uhakika wa kuchukua changamoto hii, ambayo inaweza kuwa mradi wa muda mrefu, ni kitu ambacho naweza kujitolea, lakini naitakia klabu mafanikio kwa siku zijazo na ninatumai klabu itarejea Ligi Kuu. Amesema kocha huyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Leeds United Angus Kinnear aliongeza kuwa anamshukuru Sam kwa kuwa jasiri vya kutosha kuingilia kati na kufanya kila awezalo kuwaokoa.
“Kwa kusikitisha, haikuwa hivyo, lakini Sam, Karl na Robbie walifanya kila waliloweza kuinua hali ya Thorp Arch na Elland Road na kwa hilo sote tunashukuru sana. Taarifa hiyo pia inaonyesha kuwa klabu hiyo inalenga kuwa na kocha mkuu mpya katika wiki zijazo”.

Allardyce alifanikiwa kupata pointi moja pekee katika mechi nne alizocheza kwa kuchapwa mabao 4-1 nyumbani na Tottenham na hivyo kuhitimisha hatma ya Leeds katika siku ya mwisho ya kampeni.

