Lisandro Martinez na Mkosi wa Waargentina United

Beki wa Manchester United Lisandro Martinez ameendeleza mkosi wa wachezaji wa Argentina ambao wameshindwa kutamba ndani ya klabu hiyo kutokana na majeraha ambayo amekua akiyapata.

Taarifa ambayo ilitoka jana kua beki huyo atakua nje ya uwanja kwa mwezi mmoja wakati ambao tayari ametoka kwenye majeraha akiwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili, Ambapo pia alikaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu mwanzoni mwa msimu huu.lisandro martinezBeki huyo amekua akiandamwa na majeruhi kuanzia mwishoni mwa msimu uliomalizika ambapo alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Sevilla, Majeraha ambayo yamekua yakijirudia mara kwa mara msimu huu na kumfanya kukosekana uwanjani mara kwa mara.

Beki huyo wa kimataifa wa Argentina anafata nyendo za raia wenzake wa Argentina klabuni hapo ambao walishindwa kutamba kwa sababu mbalimbali wengine wakifeli pia kwasababu ya kuandamwa na majeraha kama ambayo yanamsumbua beki huyo kwasasa.lisandro martinezWachezaji wa kimataifa wa Argentina ambao wameshindwa kutamba ndani ya Man United ni pamoja na Juan Sebastian Veron kiungo fundi huyu, Beki Gabriel Heinze, Angel Di Maria, Marcos Rojo, Huku Lisandro Martinez akianza kutabiriwa kushindwa kutamba klabuni hapo licha kua na mwanzo mzuri.

 

Acha ujumbe