Lisandro Martinez Ajiunga na Timu ya Taifa ya Argentina

Beki wa klabu ya Manchester United Lisandro Martinez ameonekana kwenye kambi ya timu ya taifa ya Argentina akifanya mazoezi na wenzake ikiwa ni taarifa nzuri kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Lisandro Martinez alikua anauguza majeraha yake ambayo aliyapata katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Westham United, Ambapo amekaa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mmoja tu.lisandro martinezBeki huyo amekua mhimili mkubwa kwa klabu ya Man United  hivo kupata kwake majeraha ilikua ni pigo klabuni hapo, Lakini baada ya kuonekana kwenye kambi ya timu ya taifa ya Argentina ni wazi yupo fiti kurejea ndani ya timu hiyo.

Baada ya mechi za kimataifa klabu ya Manchester United inaweza kupata huduma ya beki huyo ambaye alipata majeraha mwezi Febuari dhidi ya klabu ya Westham, Lakini kwasasa anaonekana yupo tayari kurejea kwenye timu.lisandro martinezHizi zitakua ni taarifa nzuri kwa benchi la ufundi la klabu ya Man United likiongozwa na kocha Erik Ten Hag, Lisandro Martinez amekua akiandamwa na majeraha sana hivi karibuni kwani mpaka sasa ameshapata majeraha mara tatu ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe