Liverpool leo wanaingia kibaruani tena dhidi ya mabingwa wa ligi kuu ya Uholanzi maarufu kama Eredivise katika dimba la Anfield.

Vijogoo hao kutoka Merseyside wanakwenda kucheza mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi barani ulaya huku wakiwa na kumbukumbu ya kupokea kipigo kizito kutoka klabu ya Napoli kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya uliopigwa katika dimba Diego Armando Madonna.

liverpoolLeo timu hiyo wanakwenda kujiuliza dhidi ya timu inayofanya vizuri kwenye michezo yake kwasasa na hata kwenye mchezo wa kwanza Ajax walishusha kipigo kizito kwa Rangers cha mabao manne kwa bila ya nchini Uskochi na leo wanakaribishwa na vijogoo hao wakiwa kwenye maumivu ya kupoteza mchezo wa kwanza.

Jambo kubwa linalosubiriwa ni je vijana wa Klopp watarudi kwenye ubora wao na kufuta makosa ya mchezo uliokwisha au Ajax wataendelea walipoishia kwenye mchezo uliomalizika.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa