Klabu ya Liverpool imekumbana na wakati mgumu baada ya kutoka kwenye wikiendi nzuri baada ya kuifunga klabu ya Manchester United kwa mabao 7-0 katika dimba la Anfield wikiendi iliyomalizika.
Liverpool wamekubali kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya klabu ya Afc Bournamouth katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza mapema leo, Katika mchezo ambao umepigwa katika dimba la Vitality na kuwafanya Vijogoo hao wa Merseyside kupigwa na butwaa.
Goli la mapema kupitia kwa mshambuliaji Philip Billing ambalo limedumu mpaka dakika ya 90 ya mchezo ndio lilipeleka kilio kwa vijogoo hao wa Merseyside, Mchezo ambao klabu ya Liverpool ilionekana kuutawala kwa kiwango kikubwa lakini wakashindwa kupata matokeo.
Afc Bournamouth baada ya kushinda mchezo wa leo wameza kusogea kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza mpaka kufikia nafasi ya 16 baada ya kufikisha alama 24, Hivo klabu hiyo imeanza kufufua matumaini yake ya kuendelea kubaki katika ligi kuu ya Uingereza.
Klabu ya Liverpool baada ya kupokea kichapo dhidi ya dhidi ya klabu ya Bournamouth kimewafanya kuendelea kusalia na alama zao 42 na kubaki nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Katika mchezo wa leo Vijogoo walikua wana nafasi ya kusawazisha bao kupitia mkwaju wa penati dakika ya 70 lakini Mohamed Salah alikosa mkwaju huo na matokeo kubaki hivo mpaka mwisho wa mchezo.

