Klabu ya Liverpool leo itashuka dimbani dhidi ya klabu ya Manchester United katika dimba la Anfield katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kuhakikisha wanalinda rekodi yao dhidi ya mashetani wekundu.
Liverpool wamekua na rekodi nzuri dhidi ya Manchester United katika dimba la Anfield kwa takribani miaka saba sasa, Klabu ya Man United wamefanikiwa kushinda katika dimba la Anfield mara ya mwisho ilikua mwaka 2016 hivo leo ni vita ya kulinda rekodi dhidi ya wanaopambana kuvunja rekodi.Klabu ya Manchester United ambayo inaonekana kua na ubora kwasasa na mfululizo mzuri wa kupata matokeo wanakwenda kucheza na vijogoo wa Anfield ambao wanaonekana kutokua kwenye ubora wao, Lakini mara nyingi vilabu hivo vinapokutana ushindani hua mkubwa bila kujalisha fomu ya mmoja wao.
Liverpool licha ya kupambana kulinda rekodi yao dhidi ya klabu ya Manchester United katika dimba la Anfield, Lakini pia watahakikisha wanafanikiwa kupata ushindi ili kuendelea kuweka hai matumaini yao kuingia kwenye nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.Klabu ya Manchester United wao leo watakua wanahitaji kuvunja rekodi ya Liverpool dhidi yao wakiwa kwenye dimba lao la nyumbani, Huku alama tatu dhidi ya Liverpool zitakua muhimu pia kwa mashetan hao wekundu ili kuendelea kubaki kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.