Mshambuliaji wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe amesema kua ndoto yake kubwa ni kushinda taji la ligi ya mabingwa ulaya ameyazungumza hayo baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Nantes usiku wa jana.

Kylian Mbappe ana ndoto kubwa ya kutwaa taji la ligi ya mabingwa ulaya licha ya kufanikiwa kutwaa mataji matano ya ligi kuu ya Ufaransa, pamoja na kushinda taji la kombe la dunia mwaka 2018 akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa lakini malengo yake yamebaki kutwaa taji la kigi ya mabingwa ulaya.mbappeMshambuliaji huyo alikaribia kushinda taji hilo mwaka 2020 baada ya kucheza fainali ya ligi ya mabingwa ulaya wakiwa chini ya kocha Thomas Tuchel, Lakini hakufanikiwa kwani walipoteza kwa bao moja kwa bila dhidi ya wababe wa Ujerumani klabu ya Bayern Munich.

Mbappe wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema anawaza kushinda taji la ulaya aliulizwa kama Bayern wameshika hatma ya yeye kubaki ndani ya PSG lakini alkanusha na kusema “Sidhani hivyo, Nadhani mustakabli wangu ni kushinda ligi ya mabingwa ulaya, lakini siwezi kufika mbali hivo naiheshimu klabu”mbappeMshambuliaji Mbappe aliweka wazi kua ana furaha ndani ya PSG na lengo lake ni kuendelea kuwapa furaha mashabiki wa klabu hiyo, Huku akikanusha kua ataondoka ndani ya klabu hiyo kama watashindwa kutwaa taji la ligi ya mabingwa ulaya ambalo ndio limekua lengo lake kw amuda mrefu sasa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa