Klabu ya Liverpool ya na Real Madrid zimeingia kwenye vita kali ya kumuwania kiungo wa klabu ya Borussia Dortmund raia wa kimataifa wa Uingereza Jude Bellingham.

Klabu ya Liverpool na kocha Jurgen Klopp amenukuliwa mara kadhaa akionesha kuvutiwa na kiungo Jude Bellingham kutoka klabu ya Borussia Dortmund, Lakini Real Madrid nao wanaelezwa kuvutiwa na kiungo huyo na yupo kwenye juu kwenye orodha ya wachezaji wanaohitajika dirisha kubwa.LiverpoolKiungo Jude Bellingham amejipandisha thamani kwa kiwango kikubwa sokoni kutokana na kiwango kizuri ambacho anakionesha ndani ya klabu ya Borussia Dortmund, Kitu kinachowafanya vigogo mbalimbali barani ulaya kuhitaji kupata saini ya kiungo huyo.

Mpaka wakati huu klabu za Liverpool na Real Madrid zimekua juu kwenye mchuano wa kumuhitaji mchezaji kiungo huyo anayefanya vizuri kwenye ligi kuu ya Ujerumani, Hivo kinachosubiriwa zaidi ni dirisha kubwa kuona ni klabu gani itanasa saini ya kiungo huyo.LiverpoolKlabu ya Manchester United ilikua kwenye kinyang’anyiro cha kumuwania kiungo Jude Bellingham, Lakini bado haijafahamika kama wapo kwenye utaratibu huo kutokana na mchakato wa klabu hiyo kuuzwa hivo hakuna uhakika wa kiwango kikubwa cha pesa kitakachotoka katika usajili dirisha kubwa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa