Ancelotti: Hatutarudia Makosa Dhidi ya Barcelona

Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema hawatarudia makosa dhidi ya klabu ya Barcelona ambayo waliyafanya katika michezo iliyopita ameyasema kuelekea mtanange wa El Clasico.

Klabu ya Real Madrid na Barcelona wanatarajiwa kucheza mchezo wa nusu fainali wa kombe la Copa de le Rey unaotarajiwa kupigwa kesho, Real Madrid wamekua wakipata shida wanapokutana na klabu ya Barcelona na mara ya mwisho Madrid walipoteza dhidi ya Barca katika fainali ya kombe la Spanish Super Cup.ANCELOTTIKocha Ancelotti amesema kua klabu ya soka ya Real Madrid ilipoteza dhidi ya Barcelona katika mchezo wa Spanish Super Cup huko Saudia Arabia, Lakini kocha huyo amesema kua makosa ya klabu hiyo katika mchezo dhidi ya Barcelona hayatajirudia tena.

Klabu ya Real Madrid imekua haipo kwenye kiwango kizuri sana msimu huu kutokana na kudondosha alama mara kwa mara, Jambo ambalo kocha Ancelotti amekiri kua hawapo vizuri sana msimu huu kama msimu uliomalizika lakini ameahidi kua mambo mazuri yanakuja.ANCELOTTIKlabu ya Real Madrid mpaka wakati huu wanashindania mataji matatu ambayo ni taji la ligi kuu nchini Hispania La liga, ligi ya mabingwa ulaya, na Copa de le Rey ambalo wanakwenda kucheza mchezo wa nusu fainali ya kombe hilo dhidi ya klabu ya Barcelona hapo kesho.

Acha ujumbe