Ancelotti Asema Vinicius Alistahili Kuwepo Kwenye Kikosi Bora

Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kua mchezaji raia wa kimataifa wa Brazil Vinicius Jr alistahili kwenye kikosi bora cha FIFA kilichotangazwa usiku wa jana kwenye ghafla ya utoaji wa tuzo za FIFA.

Mchezaji Vinicius Jr jina lake halikutokea kwenye kikosi bora cha mwaka 2022 kilichotolewa na FIFA hapo jana jambo ambao linaonekana kutokukubaliwa na watu wengi na mmoja wao ni kocha wa klabu ya Real Madrid ambaye hakusita kuweka hisia zake na kusema mchezaji wake alistahili kuwepo.ancelottiMchezaji Vinicius Jr alikua kwenye ubora mkubwa mwaka 2022 akiisaidia klabu yake ya Real Madrid kushinda taji la ligi ya mabingwa ulaya, taji la ligi kuu nchini Hispania, pamoja na kombe la Spanish Super Cup hivo alikua na kila sababu ya kuwepo kwenye kikosi hicho.

Carlo Ancelotti wakati anazungumza na wanahabari alisema “Wote tunajua kua ulistahili kuwepo pale, Lakini sasa ni muda wa kuonesha tena na unatakiwa kuanza na Barcelona” Klabu ya Real Madrid watakipiga na Barcelona kesho katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la mfalme nchini humo.ancelottiTuzo za FIFA zimeibua maswali mbalimbali baada ya kutolewa jana huku watu wengi wakionesha kutokufurahishwa na maamuzi yaliofanywa katika tuzo mbalimbali katika usiku wa jana, Hivo suala la Vinicius Jr sio jambo pekee ambalo limepigiwa kelele kwenye tuzo hiyo.

Acha ujumbe