Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelottti amesema kua winga wa kimataifa wa Brazil klabuni hapo Vinicius Jr ni miongoni mwa wachezaji hatari na mahiri sana duniani kwasasa.

Kocha Ancelotti alimvulia kofia mchezaji wake Vinicius Jr baada ya kuonesha kiwango kikubwa katika mchezo dhidi Liverpool usiku wa jana, Vinicius alifanikiwa kufunga mabao mawili jana katika mchezo huo huku akiisaidia klabu yake ya Real Madrid kushinda mabao matano kwa mawili.ViniciusWinga huyo amekua na takwimu nzuri sana kila anapokutana na liverpool mpaka sasa mchezaji huyo amekutana na Liverpool mara tano mpaka sasa akifanikiwa kufunga mabao matano na kupiga pasi moja ya bao, Hivo Vinicius ana wastani wa kufunga kila mchezo aliokutana na Liverpool.

Ancelotti aliongea na wanahabari na kuwaeleza “Leo, kwa maoni yangu ndio mchezaji mwenye maamuzi makubwa katika soka la dunia, Haachi, anapiga chenga, anatoa pasi, anafunga sasa yeye ndiye mwenye maamuzi zaidi. Tunatumaini ataendelea hivi”Vinicius anakua mchezaji wa kwanza mdogo mwenye miaka 22 na siku 224 kufunga mabao mawili katika dimba la Anfield katika michuano ya Ulaya tangu Johan Cruyff afanye hivo mwaka 1966 akiwa na miaka 19 na siku 233, Vinicius anaendelea kuboresha uwezo wake kila siku na hilo linamfanya kuanza kufikiriwa anaweza kushinda Ballon kama akiendelea hivi.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa