Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez amesema hawataihofia klabu ya Manchester United kuelekea mchezo wa marudiano wa mtoano kombe la Europa utakaopigwa katika dimba la Old Trafford Alhamisi hii.

Mchezo uliozikutanisha timu hizo Alhamisi atika dimba la Camp Nou ulimalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili, Hivo kocha Xavi haoni kama kuna sababu ya kuihofia Man United kuelekea mchezo wa marejeano kwani wanahitaji kuonesha ubora wao ili kuweza kushinda mchezo huo.XaviKocha huyo amesema atakua na furaha kucheza tena katika ardhi ya Uingereza kwani imekua jambo zuri kucheza nchini humo kutokana na mashabiki ambao wamekua wakionesha mapenzi kwa timu zao, Haswa akiuongelea uwanja wa Old Trafford ambao anasema unatakiwa kucheza angalau mara moja katika maisha yako.

Xavi alisema ” Sisi ni timu jasiri inyopenda kushambulia na kushinda kila mara, Mchezo huu hautakuwa maalumu kwani utakua kama mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya, Kwa mashabiki ni mchezo wa kuvutia, Kwa wachezaji ni mchezo ambao unahitaji kucheza angalau mara moja katika maisha yako”XaviKlabu ya Barcelona chini ya kocha Xavi ina kibarua kigumu katika dimba la Old Trafford kwani klabu ya Manchester United imeugeuza uwanja wao kama ngome tena, Kwani klabu hiyo haijapoteza mchezo wowote nyumbani tangu mwaka jana mwezi Septemba hivo ni mchezo unaotarajiwa kua mgumu na wenye mvuto kwelikweli.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa