Neymar Jr Hatihati Kuikosa Bayern Munich

Staa wa klabu ya PSG inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa Neymar Jr yuko kwenye hatihati ya kuukosa mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa ulaya kutokana na jeraha la enka alilolipata wikiendi hii.

Neymar Jr amekua kwenye ubora mkubwa msimu huu ndani ya klabu ya PSG huku akiwa moja ya wachezaji waliohusika na magoli mengi ndani ya klabu hiyo kando ya Mbappe na Messi,Lakini mchezaji huyo alipata majeraha ya enka katika mchezo wa ligi kuu ya Ufaransa dhidi klabu ya Lille ya Ufaransa.Neymar jrNyota huyo wa kimataifa wa Brazil amekua akiandamwa na majeraha sana ndani ya klabu hiyo jambo ambalo limekua likimrudisha nyuma, Staa huyo anaelezwa anaweza kukaa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu mpaka nne na hiyo inaonesha wazi mchezaji huyo ataukosa mchezo dhidi ya klabu ya Bayern Munich.

Neymar Jr kukosekana katika mchezo dhidi ya Fc Bayern Munich itakua pengo kubwa kwa klabu ya PSG kwani mchezaji huyo amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya timu hiyo, Hivo kumkosa katika mchezo mgumu dhidi ya klabu ya Bayern Munich itakua pigo kubwa.Neymar jrKlabu ya PSG itasafiri mpaka nchini Ujerumani mpaka kwajili ya kwenda kumenyana na klabu ya Bayern Munich ambapo watakua nyumbani katika dimba lao la Allianz Arena, Hivo PSG watakua kwenye kipindi kigumu kwani tayari wameshapoteza mchezo wa awali wakiwa katika dimba lao la nyumbani.

Acha ujumbe