Ten Hag Alenga Kuondoa Ukame wa Makombe Man United

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amesema hashangazwi na mabadiliko ya haraka ambayo yanaonekana ndani ya klabu hiyo lakini akisema lengo kubwa ni kuondoa ukame wa mataji ndani ya klabu hiyo.

Mpaka sasa kikosi cha Manchester United Erik Ten Hag imekua timu pekee kutoka nchini Uingereza ambayo inawania mataji yote mpaka sasa, Man United itacheza mchezo wa marudiano wa kombe la Europa dhidi ya Barcelona na Jumapili itacheza mchezo wa fainali wa kombe la Carabao dhidi ya Newcastle United na kuwinda taji lao la kwanza msimu huu.ten hagKlabu ya Manchester United haijafanikiwa kubeba taji lolote tangu mwaka 2017 walipofanikiwa kubeba taji la Europa League pamoja na kombe la Carabao wakati huo wakati huo kocha akiwa Jose Mourinho, Hivo kubeba taji msimu huu ni jambo kubwa sana ambalo litarudisha heshima ya klabu hiyo.

Kocha Erik Ten Hag anasema lengo kuu ndani ya klabu ya Manchester United sio kuimarika tu kitu kikubwa zaidi ndani ya klabu hiyo na ndio malengo ya klabu kubwa kama Man United ni mataji, Akizungumza na wanahabari leo kocha huyo anasema kitu wanachokitazamia zaidi msimu huu ni kushinda taji.ten hagKocha Ten Hag amezungumzia mchezo dhidi ya Barcelona amesema wamejipanga vizuri kuelekea mchezo dhidi ya Barcelona huku akisema wanatakiwa kua kwenye ubora wao ili kushinda mchezo huo, Lakini vilevile kocha huyo amesema anatarajia wachezaji wake wawili kuelekea mchezo wa kesho kurejea ambao ni Harry Maguire, pamoja na Antony.

Acha ujumbe