Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema yeye na wachezaji wake hawana wasiwasi juu ya mazungumzo yanayoendelea ya kumtafuta mmiliki mpya wa klabu hiyo.

Kocha Erik Ten Hag amesema kua hawaruhusu mchakato wa kupata mmiliki mpya klabuni hapo uwavuruge yeye na wachezaji wake, Kwani suala hilo lipo nje yao na kazi yake yeye ni kuhakikisha anapata matokeo katika michezo ambayo ipo mbele yao.Ten HagKlabu ya Manchester United ambayo ipo sokoni na siku mbili nyuma ilikua siku ya mwisho kwa wanunuzi kupeleka ofa zao na mpaka sasa matajiri wawili ndio wanaowania klabu hiyo ambao ni Jim Ratcliffe raia wa Uingereza na Jasim Bin Hamad bin Al Thani kutoka nchini Qatar.

Kocha Ten Hag amesema kua mpaka sasa mipango yao ipo kwenye michezo ambayo inafuata hasa katika wiki inayofuata ambayo itakua ngumu zaidi, Kwani kuna mchezo w amarudiano dhidi ya klabu ya Barcelona na mchezo wa fainali dhidi ya klabu ya Newcastle United.Ten HagKocha Ten Hag anasema kua suala linaloendelea nje ya uwanja kwasasa halimuhusu yeye kwani anachojua yeye kazi yake ni kuisimamia klabu hiyo na kuhakikisha inapata matokeo,Lakini kocha huyo aligusia suala la kumuongezea mkataba mchezaji huyo na kusema ni kipaumbele chao na wanalifanyia kazi.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa