Klabu ya Chelsea wapo kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba kiungo wake mashuhuri klabuni hapo Ngolo Kante ili aweze kuendelwa kusalia katika viunga vya Stamford Bridge.

Chelsea wanaripotiwa wanaendelea na mazungumzo na Kante iliwaweze kumuongezea Mkataba kiungo huyo ambaye amekua nje ya uwanja kwa muda mrefu msimu akiandamwa na majeraha, Lakini ameonekana kurejea kwenye kiwanja cha mazoezi ndani ya klabu hiyo.ChelseaKiungo Ngolo Kante inafahamika kua mkataba wake wa kuendelea kuwatumikia matajiri wa hao wa London unamalizika mwishoni mwa msimu, Na ndio maana klabu hiyo inapambana sana kuhakikisha wanampa mkataba mpya kiungo huyo wa shoka kabla ya msimu kumalizika.

Taarifa zinaeleza kua tayari kuna makubaliano ya pande zote mbili baina ya Kante na klabu ya Chelsea, Huku kinachosubiriwa mpaka sasa ni kutambua urefu wa mkataba ambao utakua umesainiwa utamuweka mchezaji huyo klabuni hapo kwa muda gani.ChelseaSiku zote kipaumbele cha Kante ni kusalia ndani ya klabu ya Chelsea kinachosubiriwa ni mambo muhimu ya kimkataba kukamilishwa huku mazungumzo yakiendelea baina ya zote mbili, Kiungo ni moja ya viungo wenye heshima kubwa ndani ya klabu hiyo kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha klabuni hapo toka amejiunga na klabu hiyo mwaka 2016.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa