Kiungo wa klabu ya Manchester City Kevin De Bruyne atakosekana katika mchezo wa leo kati ya klabu yake dhidi ya klabu ya Rb Leipzig ya Ujerumani katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya hatua ya 16 bora.

Mchezaji Kevin De Bruyne atakosekana leo dhidi ya Leipzig ikiwa ni taarifa ya kushtua kwa mashabiki wa klabu ya Manchester City kwani mchezaji huyo alikuwepo kwenye mchezo wa wikiendi dhidi ya klabu ya Nottingham Forest lakini ghafla inataarifiwa kua atakosekana katika mchezo wa leo.kevin de bruyneKlabu ya Manchester City ambayo imesafiri mpaka nchini Ujerumani kwajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Rb Leipzig ambapo vijana wa Pep Guardiola watakua ugenini katika dimba la Red Bull Arena wakitupa karata yao ya kwanza katika mchezo huo wa hatua ya 16 bora.

Kocha Pep Guardiola aliweza kuthibitisha kukosekana kwa Kevin De Bruyne punde tu ya kutua Ujerumani kua kiungo huyo alipata matatizo ya kiafya, Hivo kocha huyo amethibitisha kukosekana kwa nyota huyo pamoja na beki Aymeric Laporte ambaye pia nae amepata matatizo ya kiafya.kevin de bruyneKevin De Bruyne amekua mhimili wa klabu ya Manchester City kwa kipindi kirefu akitengeneza mabao na kufunga mabao pale ambapo anakua anahitajika kufanya hivo, Kukosekana kwake katika eneo la katikati la klabu hiyo ni wazi kunaacha pengo kubwa ambalo itakua vigumu kidogo kuzibika.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa