Sabitzer Anataka Kubaki Man United

Kiungo wa klabu ya Fc Bayern Munich Marcel Sabitzer ambaye yupo kwa mkopo ndani ya klabu ya Manchester United taarifa zinaeleza kiungo anatamani kuendelea kubaki ndani ya viunga vya Old Trafford.

Marcel Sabitzer inaelezwa kua anatamani sana dili lake la kujiunga na klabu ya Manchester United kwa mkataba wa kudumu baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika mwishoni mwa msimu huu, Lakini hii itategemeana na makubaliano ya klabu ya Bayern Munich na Manchester United.sabitzerSiku za karibuni wakala wa kiungo huyo wa kimataifa kutoka Austria alisema hatma ya kiungo itajulikana mwishoni mwa msimu huu, Lakini kwa taarifa ambazo zipo mchezaji huyo anataka kusalia katika jiji la Manchester kuendelea kuwatumikia mashteni wekundu.

Kiungo Marcel Sabitzer amekua kwenye ubora ndani ya Manchester United tangu amejiunga kwenye timu hiyo, Alifanikiwa kucheza kwa kiwango kizuri katika michezo mitatu ambayo kiungo Casemiro alikua ana adhabu ilionesha ubora wa kiungo huyo.sabitzerMarcel Sabitzer inaelezwa kuhitaji kucheza kwa kiwango kizuri chini ya kocha Erik Ten Hag ili kuweza kumshawishi kocha huyo, Kwani hata mchezaji huyo akihitaji kubaki Old Trafford lakini asilimia kubwa watakaemua ni klabu ya Manchester United kama watavutiwa na mchezaji huyo.

Acha ujumbe