Gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole amemwagia sifa kiungo wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Brazil Carlos Casemiro na kusema amebadilisha timu hiyo kwa kiasi kikubwa.

Cole anamuona Casemiro kama mchezaji ambaye ameleta mabadiliko makubwa ndani ya kikosi cha Manchester United, Kwani kiungo huyo amekua akionesha utofauti siku hadi siku kwenye kikosi hicho chini ya Erik Ten Hag bna kufanya kupokea sifa lukuki kutoka kwa gwiji huyo.CasemiroAndy Cole anasema klabu ya Manchester United kila siku ilikua inatarajia kupata kiungo wa ulinzi mwenye ubora mkubwa, Lakini wengi hawakutarajia kuona kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid anacheza kwenye kiwango cha juu kiasi ambacho anakionesha kwasasa ndani ya klabu hiyo.

Kiungo Casemiro ambaye amejiunga na miamba hiyo ya soka nchini Uingereza kwenye dirisha kubwa lililopita amekua moja ya wachezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Manchester United, Kwnai hata pale anapokua anakosekana klabu hiyo ilionekana kutetereka.CasemiroManchester United wamekua wakipitia kipindi kigumu kwenye eneo la kiungo wa ulinzi tangu alipoondoka Michael Carrick, Lakini Casemiro amekuja kuonesha ubora wa hali ya juu ndani ya timu hiyo hadi magwiji wa klabu hiyo kama Cole wanashangazwa na ubora ambao anauonesha ndani ya timu hiyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa