Kiungo wa klabu ya Manchester United Carlos Casemiro anasema kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag ni kocha ambaye anapenda kushinda kila siku na anahitaji wachezaji wajitume kwelikweli.

Kiungo Casemiro binafsi anasema anavutiwa na tabia ya kocha wake kwani kama kocha unatakiwa kutaka kushinda ila siku na kuweza kufikia malengo, Vilevile kocha huyo inaelezwa anahitaji wachezaji wake wajitume zaidi kila siku na kua wapambanaji na kuisaidia timu kufika ambapo wanahitaji.CasemiroKocha Ten Hag amekua akisifika kama kocha mwenye mbinu nzuri lakini pia amekua kocha ambaye anapenda wachezaji wake wajitume na kusimamia misingi ya nidhamu zaidi ndani ya timu hiyo, Kwani anaamini wachezaji wake wakijituma ndio sababu ya kuweza kufanikiwa.

Casemiro amewahi kunukuliwa pia akisema katika makocha ambao wamewahi kumfundisha basi Ten Hag ni kocha ambaye ni mshindani sana na anahitaji kushinda kila siku, Hivo tabia ya kocha huyo imemvutia kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil.CasemiroKocha Ten Hag amefanikiwa kubadilisha klabu ya Manchester United kwa kiwango kikubwa kwa kipindi kifupi ambacho amekaa klabuni hapo, Mpaka sasa klabu ya Man United imefanikiwa kukaa nafasi tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza huku vilevile wakiwa wanagombea makombe yote mpaka sasa ikiwa klabu pekee kutoka Uingereza.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa