Klabu ya Arsenal imeendelea kujiimarisha kileleni baada ya kuitandika klabu ya Leicester City katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa katika dimba la King Power jioni hii.
Goli la Gabriel Martinelli mapema kipindi cha pili limepeleka kilio kwa klabu ya Leicester City na kujikuta wakipoteza mchezo wa pili mfululizo katika ligi kuu ya Uingereza, Kwani wiki iliyomalizika walipoteza dhidi ya klabu ya Manchester United kwa mabao matatu kwa bila.Vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza walifanikiwa kutandaza kandanda safi licha ya kua ugenini na kuweza kupata matokeo ambayo yanawafanya kuendelea kushika usukani kunako ligi kuu ya Uingereza wakifanikiwa kufikisha alama 57, Huku klabu ya Manchester City wakiwa na alama zao 52.
Arsenal wamekua kwenye msimu bora sana katika ligi kuu ya Uingereza huku wakiwa vinara mpaka wakati huu mchezo wa leo unakua mchezo wa pili mfululizo kwa klabu hiyo kushinda baada ya kupitia kipindi kigumu cha kutokupata matokeo katika michezo minne mfululizo.Klabu ya Arsenal inatarajia kucheza mchezo wake wa kiporo siku ya jumatano dhidi ya klabu ya Everton ambao waliwafunga katika mchezo wao wa mwisho, Hivo vinara hao baada ya kumenyana na Everton sasa watakua sawa na vilabu vingine kwa michezo.