Klabu ya Simba hatimaye hapo jana imepata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano ya Klabu bingwa wakiwa ugenini baada ya kumtandika Vipers bao 1-0 ambalo lilifanya timu hiyo kupata pointi tatu.

 

Simba Yaipasua Vipers Nyumbani Kwake

Simba ilipoteza mechi zake mbili za awali nyumbani na ugenini na hivyo kupoteza pointi sita za mwanzo kwenye kundi na jana ndipo safari yao ya ushindi ikaanzia hapo kwa bao la Henock Inonga dakika ya 20.


Baada ya ushindi huo mnyama anashikilia nafasi ya 3 kwenye kundi huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Raja Casablanca ambaye ametoka kupata ushindi dhidi ya Horoya na kukusanya alama 9.

Timu hiyo ambayo ipo chini ya kocha mkuu Roberto walifanya mashambulizi ya kutosha kwenye lango la Vipers huku mashuti matano yakilenga lango, wakati mwenyeji akipiga moja.

Simba Yaipasua Vipers Nyumbani Kwake

Mlinda mlango wa Vipers aliokoa mipira ya hatari iliyokuwa ikielekea golini mara nne huku Aishi Manula akiokoa mpira mmoja tuu ambao ulilenga lango.

 

 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa