Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi amewatafsiri Real Madrid kama wapinzani wagumu na kusema anawapa nafasi vijana wa Ancelotti kutinga fainali kuelekea mchezo wa El Clasico kesho hatua ya nusu fainali kombe la Copa de le Rey.
Mchezo kati ya Real Madrid na Barcelona unatarajiwa kupigwa kesho katika kombe la Mfalme nchini Hispania, Huku ukitarajiwa kua na mikondo miwili lakini mchezo wa kwanza unatarajiwa kupigwa katika dimba la Santiago Bernabeu kesho Alhamisi.Kocha Xavi amefanikiwa kushinda michezo miwili kati ya minne aliyokutana na Real Madrid tangu akabidhiwe timu hiyo, Huku katika michezo hiyo alifanikiwa kushinda mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza na mchezo wa pili waliifunga Real Madrid mabao 3-1 katika fainali ya kombe la Spanish Super Cup.
Kocha Xavi wakati anazungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo alisema kua Real Madrid wana nafasi kubwa kuelekea mchezo huo kutokana na kua mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Hispania, Hivo ni wazi nafasi kubwa wanapewa klabu hiyo.Licha ya klabu ya Barcelona kuongoza kwa alama saba kileleni dhidi ya klabu ya Real Madrid katika ligi kuu nchini Hispania, Lakini Xavi bado anaamini kua Real Madrid ni wapinzani wagumu na yeye kuwapa nafasi kuelekea mchezo wa nusu fainali kombe la mfalme mkondo wa kwanza.