Manchester United Kuuzwa Mwishoni mwa Msimu

Taarifa zinaeleza kua klabu ya Manchester United inatarajiwa kuuzwa mwishoni mwa msimu huu kutokana na wamiliki wa klabu hiyo kuamua mchakato wa kuiuza klabu hiyo usogezwe mbele.

Klabu ya Manchester United iliwekwa sokoni tangu mwishoni mwa mwaka jana baada ya familia ya Glazers ambao ndio wamiliki wa klabu hiyo kuamua kuipiga bei klabu hiyo, Lakini taarifa ambayo imetoka ni kua mchakato wa kuiuza klabu hiyo umesogezwa mpaka mwishoni mwa msimu huu.mANCHESTER UNITEDMatajiri wawili ambao walipeleka ofa ya kuinunua klabu hiyo ambao ni mwingereza Jim Ratcliff na Jasim Bin Hamd Emir Al Than kutoka Qatar inaelezwa ofa zao hazijafika dau ambalo wanataka wamiliki wa klabu hiyo, Inaelezwa kua matajiri wamefikia dau la bilioni 4.5 lakini wamiliki wakihitaji kiasi cha bilioni 6.

Hizi zinaweza kua taarifa mbaya kwa mashabiki wa klabu ya Manchester United ambao kwa kipindi kirefu wamekua wakihitaji matajiri hao waiachie timu hiyo kwa kile wanachodai wameshindwa kuiongoza klabu hiyo na kufanya ipoteze mvutyo wake kutokana na kufanya vibaya.mANCHESTER UNITEDTaarifa za ndani zinaeleza inaeleza kua familia ya Glazers ambao ndio wamiliki wa klabu ya Manchester United ni kua hawana utayari tena kuiuza timu hiyo, Kwa kile ambacho wanaamini kua klabu hiyo inaweza kurejesha makali yake chini ya kocha Ten Hag na kuwafanya kuepuka presha za mashabiki wa klabu hiyo.

Acha ujumbe