Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema hapotezi hata sekunde kufikiria kushinda mataji matatu ndani ya msimu huu kama ambavyo watu wengi wanafikiri timu hiyo inaweza kushinda mataji matatu.
Kocha Guardiola alizungumza hayo akiongea na wanahabari baada ya kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wa jana dhidi ya klabu ya Bristol katika mchezo wa kombe la Fa, Huku mabao ya klabu hiyo yakifungwa na Phil Foden aliyefunga mabao mawili na Kevin De Bruyne kufunga bao moja na kusaidia timu hiyo kutinga hatua ya robo fainali.Kocha huyo alipoulizwa kuhusu kushinda mataji matatu ndani ya msimu mmoja aliruka na kupinga vikali “Hapana, Sahau sahau. Unapoanza kuzungumzia hilo unaanza kupoteza mashindano na kuacha mashindano hatuko tayari. Hatutatumia hata sekunde moja kufikiria hilo, Tutatumia muda kufikiria michezo inayofuata.
Guardiola ambaye ana uzoefu wa kushinda mataji matatu ndani ya msimu mmoja akiwa na klabu ya Barcelona katika msimu wa 2008/09 akifanikiwa kubeba taji la La liga, ligi ya mabingwa ulaya, na taji la Copa de le Rey hivo inaonekana na msimu huu anaweza kufanya jambo hilo.Klabu ya Manchester City mpaka sasa inawania mataji matatu kwani klabu hiyo bado ipo kwenye kinyang’anyiro cha kuwania taji la ligi kuu ya Uingereza, ligi ya mabingwa ulaya, na kombe la Fa ambapo walifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali hapo jana lakini kocha Guardiola hataki kufikiria kuhusu kushinda mataji matatu.