Luis Enrique anaamini kwamba kiwango cha Uhispania katika kipindi cha kwanza kilikuwa kibaya baada ya kupokea kichapo siku ya Jumamosi dhidi ya Uswizi.

 

Luis Enrique Achanganyikiwa Baada ya Kupoteza Dhidi ya Uswisi

Uhispania ililala kwa 2-1 mjini Zaragoza na kuwaacha Ureno nyuma kwa pointi 2 katika kundi la A2 la ligi ya Mataifa kuelekea mchezo wa mwisho. Mechi hiyo ya mwisho ya kundi hilo itakuwa Jumanne huku Uhispania ikijiandaa kukabiliana na vinara mjini Braga, huku timu ya Fernando Santos ikishinda 4-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech Jumamosi.

Luis hakuweza kuficha kusikitishwa kwake na mchezo huo. “Kupoteza siku zote ni jambo la kuumiza. Imekuwa ni jambo la kusikitisha, lakini lazima tuithamini Uswis, ambao tangu mwanzo walituletea matatizo mengi” Kocha huyo alisema.

Luis Enrique Achanganyikiwa Baada ya Kupoteza Dhidi ya Uswisi

Alipoulizwa ikiwa mchezo huo ulizua mashaka kuhusiana na Qatar 2022, Luis alijibu “Hakuna Shaka”. Ni wazi ni bora kwenda Qatar mfululizo, lakini nina imani na timu, nimeona wachezaji wengi kipindi cha kwanza wamekuwa wakifanya makosa kuliko hapo awali, lakini wapinzani ni wazuri, wanajua joinsi wanavyocheza.

“Ushindi dhidi ya Ureno itakuwa njia mwafaka ya kufika kombe la Dunia. Tumetoka sare nao mara tatu na sasa tutaenda huko kushinda.” Ureno inahitaji sare pekee Jumanne ili kujihakikishia nafasi yao katika fainali za ligi ya Mataifa kwa mara ya pili.

Luis Enrique Achanganyikiwa Baada ya Kupoteza Dhidi ya Uswisi

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa