Bondia anayefanya vizuri kwa sasa nchini Tanzania, Selemani Kidunda jana usiku alionekana ulingoni akimpa maelekezo ya kufanya Twaha Kiduku wakati wa pambano likiendelea.

 

Kidunda Aonekana Kumpa Mbinu Twaha

Katika Pambano hilo Bondia Kutoka Nchini Misri Abdo Khaled maarufu kama Monster alionekana kumzidi mbinu mpinzani wake Twaha kwa kuwa mjanja sana wakati wa kurusha ngumi, na kuhama kutoka nafasi moja kwenda nyingine.

 

Kidunda Aonekana Kumpa Mbinu Twaha

Mpaka raundi ya sita Kiduku alionesha mchezo mzuri kwa kumpiga mpinzani wake ngumi za mfululizo na kumfanya apunguze kasi yake aliyoaanza nayo kwenye raundi tano za mwanzo.
Twaha aliweza kumpiga mpinzani wake up cut na kuendelea kuushika mchezo kwa raundi ya sita na saba na Abdo Khaled akawa haelewi cha kufanya mpaka mapumziko Uwanja ulikuwa ukishangilia uchezaji wa bondia huyo.

 

Kidunda Aonekana Kumpa Mbinu Twaha

Na mpaka raundi ya 10 ambayo ndio ilimfanya bingwa wa mkanda wa UBO Afrika Mabara kupatina ambaye ni Kiduku akishinda kwa alama 99-90, 99-90, 100-89

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa