MANDONGA:Lile pambano lililosubiliwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa ndondi, Kati ya Karim Mandonga mtu kazi dhidi ya Salim Ally kutoka Tanga lenye hadhi ya uzani wa kati, lilifanyika jana usiku mkoani mtwara na kulazimika kumalizika kwa sintofahamu.

Pambano hilo la raundi 4, lilianza kwa kasi kubwa kila mmoja akijaribu kurusha makonde ya kutosha kwenda kwa menzake.

 

mandonga, Pambano la Mandonga Limeisha kwa Utata., Meridianbet

Kwa Raundi tatu za kwanza Bondia wa Ngumi Mchomoko alionekana kutawala pambano huku akiwafurahisha mashabiki zake kwa mbwembe nyingi.

Hali ilibadilika kwenye raundi ya Mwisho ambapo Salim aliamka kutoka usingizini na kuanza kujibu mashambilizi kwa kasi kubwa na kufanikiwa kumdondosha mara mbili karim, lakini mwamuzi wa kati alishindwa kumhesabia na kuruhusu pambano liendelee hali ambayo ilisababisha mwenyekiti wa bodi ya ngumi za kulipwa Chaurembo Pawasa kulifuta pambano.

“Mimi natoka bodi ya ngumi za kulipwa, nimelazika kulifuta pambano hili kwa sababu za kushindwa kufuata sheria za “Boxing” hivyo hakuna bingwa wa pambano” Alisema Pawasa.

 

Pambano la Mandonga Limeisha kwa Utata.

Mara baada ya pambano hilo kufutwa mabondia wote walipata nafasi ya kuzungumza ambapo Salim alisema kuwa pambano lilikuwa zuri, na alicheza vizuri.

Nae Karim Alisema kuwa yeye ni mtu kazi, hivyo mara ya pili bandia kama yule (Salim) atafia uwanjani.

 

Pambano la Mandonga Limeisha kwa Utata.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa