Raphael Varane amesema kuwa wachezaji katika kambi ya Ufaransa wana wasiwasi baada ya kaka yake Paul Pogba anayejulikana kwa jina la Mathias Pogba kushitakiwa kwa madai ya kujaribu kumnyang’anya kiungo huyo mali zake.
Pogba hayupo kwenye kikosi cha Ufaransa mpaka sasa kutokana na jeraha, na nafasi yake ya kucheza Kombe la Dunia iko kwenye mizani. Hata hivyo yamekuwa mambo ya nje ya uwanja ambayo yamechukua tahadhari hivi karibuni kuhusu mchezaji wa Juventus.
Uchunguzi ulifunguliwa mwezi Agosti dhidi ya tuhuma kwamba Pogba alikuwa mlengwa wa njama hizo za unyang’anyi ya kaka yake Mathias na marafiki zake wa utotoni wakidai kiasi cha Euro Milioni 13.
Mathias, ambaye ni mcheza huru baada ya kucheza na timu ya daraja la nne ya Ufaransa Belfort kumalizika mwezi April, alitishia kusambaza video iliyokuwa imetupiwa katika mtandao wa kijamii.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 32 amekana mashitaka hayo, lakini yeye na wengine wanne walishitakiwa hivi karibuni kutokana na suala hilo. Alipoulizwa kuhusu kama wachezaji wa Ufaransa wanamzungumzia Pogba Varane alisema;
“Kwa bahati mbaya kuna habari nyingi zisizo za kimichezo kwa sasa. Tunajaribu kuwa makini uwanjani. “Kama mchezaji, hilo ndilo lazima litangulie, lakini hatuko makini na kile kinachotokea karibuni nasi. Hasa inapohusisha mtu unayemfahamu, Pia tunahisi wasiwasi kwa namna fulani”.
Varane aliendelea kwa kusema kuwa kwa ndani wanaendelea vizuri sana, wanazingatia lengo lao na wanajaribu kuwa wataalamu iwezekanavyo.
Varane na Pogba walikuwa wanacheza katika timu moja ya Manchester United msimu uliopita, kabla ya Pogba kutimkia Juventus baada ya kumalizika kwa mkataba wake Old Traford, na kuanza kwa mara ya pili Juventus.
Kocha mkuu wa Ufaransa Didier Deschamps amesema kuwa hatakerwa na matukio yanayoendelea nje ya uwanja, anapotayarisha timu yake kujiandaa kumenyana na Denmark siku ya leo, kwenye ligi ya Mataifa.