Mwanamasumbi ambaye amejipatia umaarufu kwa kipindi kifupi kwenyemchezo wa ngumi baada ya kupoteza mapambano yake mawili yaliofanikiwa kuoneshwa na kutizamwa na wengi nchini Tanzania Karimu Mandonga hatimaye leo amefanikiwa kushinda kwa TKO.

Mandonga kwenye pambano hilo, alikuwa akipigana na Musa Omary. Pambano hilo liliandaliwa na wizara ya sanaa na michezo kwa kushirikiana na BASATA kwa ajiri ya kuhamasisha sensa.

Mandonga, Mandonga Apiga Mtu Round ya Kwanza kwa T.K.O, Meridianbet

Pambano kati ya Mandonga na Omary lilikuwa sehemu ya kampeni ya serikali ya kuhamasisha wananchi wake kupitia michezo kwa ajiri ya faida ya kuhesabiwa tarehe 23 na wala halikuwa pambano la ushindani.

Mandonga kwenye karenda yake anatarajia kurudi Ulingo mwezi wa tisa ambapo tarehe rasmi bado haijawa wazi ili kurudisha alichopoteza baada ya kupigwa mara mbili mfululizo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa