Kocha wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel hana haraka ya kurudi tena sokoni ili kuimarisha kikosi chake kwa kuingiza maingizo mapya ya wachezaji ili kuimarisha kikosi hicho kilichopoteza kwenye mchezo wa leo dhidi ya Leeds kwa goli 3-0.

Awali Tuchel alinukuliwa kuwa alikuwa anaangalia uwezekeno wa kupata wachezaji wa daraja la juu kwenye nafasi ya mlinzi wa kati na mshambuliaji kwenye kikosi chake lakini hawezi kurupuku kununua kwa kupaniki.

Tuchel, Tuchel Hana Haraka Kurudi Sokoni, Meridianbet

Mpaka sasa klabu ya chelsea imesajiri wachezaji wachache kuliko wachezaji waliondoka ambapo wamefanikiwa kumsajiri Kalidou Koulibaly kutoka napoli huku  Antonio Rudiger na Andreas Christensen wakiondoka bure kwenye dirisha hili.

“Dirisha la usajiri bado liko wazi na litakuwepo na kuwepo na tunachohitaji ni kungalia nini tunacho na nini tunaweza fanya,” Tuchel alimwambia mwandishi baada ya mchezo wao dhidi ya Leeds

 

 

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa