Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa klabu yake itabidi ipewe pointi ikiwa mchezo wao dhidi ya Manchester United ukihairishwa kwa sababu ya mashabiki wa klabu hiyo kuandamana kupinga umiliki wa familia ya Glazer kwenye klabu hiyo.

Msimu uliopita kwenye mchezo uliowakutanisha klabu hizo wakati ya marufuku ya kutokuingia uwanjani kwenye kipindi cha korono, mashabiki wapatao 200 walijipenza ndani na kuingia uwanjani huku waengine nje wakiandamana na kupelekwa mchezo huo kuahirishwa.

Jurgen Klopp, Jurgen Klopp: Liverpool Wapewe Pointi Dhidi ya Man United, Meridianbet

Maandamano mengine yamepngwa kufanyika ya siku ya jumatatu kwenye mchezo huo, Jurgen Klopp amedai kuwa timu yake haipaswi kuadhibiwa kwa kupangiwa tarehe nyingine ya mchezo huo ikiwa mchezo huo wa jumatatu hautachezwa.

“Mipango ya mechi ya kutochezwa? Ndio, tutakwenda nyumbani na bus. Alisema Jurgen Klopp. “Kiukweli natumai isitokee lakini ikitokea nadhani tutapata pointi.

“Hatuna jambo tunaweza kufanya ikiwa mashabiki hawataki mchezo uchezwe, basi hatuwezi kupangiwa tarehe nyingine tena ya mchezo na ikawa sawa na pengine ukawa msimu wa pilipilika nyingi.

‘Watu wanatuambia kuko sawa, tunaenda kule kucheza mechi na natumaini  na tutarudi nyumbani. lakini kwenye swala kama hili, mara zote kuna kuna timu inapaswa kupewa pointi kwa sababu wao hawa kitu cha kuweza kufanya kwenye hilo na wamejianda kwa hilo.”

Jurgen Klopp ankwenda kwenye mchezo huo huku akiwa na majeruhi saba ya wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao ni Joel Matip, Ibrahima Konate, Diogo Jota and Thiago. Huku mshambuliaji wake mpya Darwin Nunez akiwa anatumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mechi dhidi Crystal Palace.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa