Mkongwe wa ndondi Mike Tyson (56) ameonekana akiwa mdhoofu kwenye kiti cha magurudumu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Miami Nchini Marekani hapo jana.

Tyson ambaye ni mmoja wa mabondia waliofanikiwa sana kwenye mchezo huo Duniani alistaafu mwaka 2005, hata hivyo amekuwa akirudi ulingoni mara kadhaa katika mfumo wa maonyesho.

tyson, Tyson Azua Gumzo Mtandaoni, Meridianbet

Taarifa zinasema kuwa Tyson anasumbuliwa na matatizo ya mgongo yanayotokana na jeraha. Hivi karibuni akiwa jijini New York bondia huyo mstaafu alihitaji kutumia fimbo ili kuweza kupata balansi ya kutembea.

Picha hizi zimezua wasiwasi kati ya mashabiki zake baada ya hivi karibuni Tyson kuutabiri mwisho wake kupitia kipindi cha HotBoxin ambapo alisema.

”wote tutakufa siku moja bila shaka. Nikijiangalia kwenye kioo, nayaona mabadiliko usoni mwangu, hii inaamaanisha tarehe ya kumalizika kwangu iko karibu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa