Bondia wa Kitanzania Twaha Kiduku amefanikiwa kuwa bingwa wa UBO Afrika Mabara kwa kumshinda bondia mwenzake Abdo Khaled Maarufu kama Monster raia wa Misri kwa pointi, baada ya raundi zote kumi kukamilika.

 

Twaha Kiduku Bingwa wa UBO

Katika Pambano hilo Bondia Kutoka Nchini Misri Abdo Khaled maarufu kama Monster alionekana kumzidi mbinu mpinzani wake Twaha kwa kuwa mjanja sana wakati wa kurusha ngumi, na kuhama kutoka nafasi moja kwenda nyingine.

Mpaka raundi ya sita Twaha alionesha mchezo mzuri kwa kumpiga mpinzani wake ngumi za mfululizo na kumfanya apunguze kasi yake aliyoaanza nayo kwenye raundi tano za mwanzo.
Twaha aliweza kumpiga mpinzani wake up cut na kuendelea kuushika mchezo kwa raundi ya sita na saba na Abdo Khaled akawa haelewi cha kufanya mpaka mapumziko Uwanja ulikuwa ukishangilia uchezaji wa Twaha.

 

Twaha Kiduku Bingwa wa UBO

Na mpaka raundi ya 10 ambayo ndio ilimfanya bingwa wa mkanda wa UBO Afrika Mabara kupatina ambaye ni Twaha Kiduku akishinda kwa alama 99-90, 99-90, 100-89

“Twaha ni bondia mzuri, amecheza pambano zuri usiku wa leo na hii itamfanya yeye asonge mbele zaidi” Abdo Khaled

 

Twaha Kiduku Bingwa wa UBO

“Boksi si mchezo wa nguvu ni mchezo wa kutumia akili” Abdo Khaled.

Kwa upande wa Twaha “Ni bondia mzuri, toka nimeanza kupigana sijawahi kuleta bondia mbovu, nawashukuru wote waliofanikisha mimi kuwa bingwa”

“Siku zote bondia anayekimbia sana kumpiga kwa KO ni ngumu, kwa jinsi alivyopigana Abdo ilikuwa ngumu kwangu kushinda kwa KO, hivyo nililazimika kumsubiri mpaka mwisho” Twaha Kiduku

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa