Kiungo wa klabu ya Brighton hove and Albion na timu ya taifa ya Argentina Alex Mac Allister anatarajiwa kuondoka klabuni hapo huku vigogo mbalimbali wakitajwa kuvizia saini yake kama Liverpool, Man United, na Chelsea.
Klabu ya Brighton inaelezwa iko tayari kumuuza mchezaji huyo dirisha hili kubwa na wanajiandaa kutangaza bei ya mchezaji huyo ambaye anafatiliwa na baadhi ya vigogo wa soka nchini Uingereza ambao tayari wanaelezwa kufanya mawasiliano na kambi ya Mac Allister huyo kwajili ya kumpata kingo huyo.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Argentina amekua akifanya vizuri ndani ya klabu ya Brighton na ku moja ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha kocha De Zerbi, Lakini ameweka wazi ataondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni msimu huu na kutimkia klabu nyingine ambayo ifafika bei ya kumnunua klabuni hapo.
Alex Mac Allister amepata jina zaidi na kuanza kufuatiliwa zaidi baada ya kufanya vzuri kwenye michuano ya kombe la dunia na timu ya taifa ya Argentina mwaka 2022 na kuweza kutwaa kombe hilo akiwa moja ya wachezaji muhimu wa kikosi cha kocha Lionel Scaloni.
Klabu ya Manchester United wanaelezwa kua karibu zaidi kambi ya Mac Allister wakifanya mazungumzo ya kumsajili kiungo huyo fundi, Man United wanaelezwa kuhitaji kiungo mwingine kwenye dirisha kubwa na miongoni mwa majini yaliyopo kwenye orodha ya timu hiyo ni raia huyo wa Argentina.

