Manchester City Yakaribia Kumbeba Gvardiol

Klabu ya Manchester City imefikia kwenye hatua nzuri ya kumsajili beki wa kimataifa wa Croatia anayekipiga klabu ya Rb Leipzig inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani Josko Gvardiol.

Manchester City wanaripotiwa kukubaliana na Josko Gvardiol maslahi binafsi mpaka sasa, Huku Leipzig wakisubiri ofa mezani kutoka kwa matajiri hao kutoka jiji la Manchester ambayo inatarjiwa kutumwa mapema wiki kesho.Manchester CityJosko Gvardiol anaripotiwa kua kwenye orodha ya juu kabisa katika klabu ya Man City na akiwa kipaumbele cha kocha Pep Guardiola ambaye anavutiwa na uchezaji wa beki huyo wa kimataifa wa Croatia kwajili ya kuboresha kikosi chake msimu ujao.

Manchester City wanatarajia kumuachia beki wake wa kati Aymeric Laporte raia wa kimataifa wa Hispania, Hivo lazima waingio sokoni kutafuta mbadala wa beki huyo na Gvardiol amekua chaguo la kwanza kabisa la klabu hiyo.Manchester CityJosko Gvardiol inaelezwa alikubaliana na Manchester City tangu dirisha dogo na kilichosubiriwa ni majira haya ya joto ili kumpata beki huyo, Josko Gvardiol amekua kwenye ubora mkubwa sana ndani ya Leipzig pamoja na timu ya taifa ya Croatia na vilabu kadhaa vilionesha kumuhitaji lakini City wameonekana kushinda mtanange huo.

Acha ujumbe