Klabu ya Manchester United itawakaribisha klabu ya Nottingham Forest leo katika mchezo wa kombe la Carabao hatua ya nusu fainali utakaopigwa katika dimba la Old Trafford.
Klabu ya Manchester United ilifanikiwa kushinda mabao matatu katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliopigwa katika dimba la City Ground jijini Nottingham. Leo vijana wa Steve Cooper watakaribishwa katika dimba la Old Trafford.
Klabu ya Nottingham Forest ambayo ilikubali kipigo cha mabao matatu kwa bila katika dimba lake la nyumbani, Leo inasubiriwa kama itaweza kupindua meza mbele ya mashetani wekundu na kuwafuata klabu ya Newcastle kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa katika dimba la Wembley mwezi huu tarehe 26.
Manchester United wao wako kwenye mawindo yao ya kuhakikisha wanarudisha heshima ndani ya klabu hiyo na kuhakikisha wanakwenda fainali ili kubeba taji hilo, Kwanin klabu hiyo haijafanikiwa kubeba taji lolote tangu mwaka 2017 ikiwa ni miaka sita sasa imeshapita.
Klabu ya Manchester United mpaka sasa wana nafasi kubwa ya kufika hatua ya fainali ya kombe la Carabao kutokana na matokeo ambayo waliyapata katika mchezo wa awali, Hivo kuna matumaini ya kwenda kucheza na klabu Newcastle ambao tayari wameshafuzu hatua ya fainali ya michuano hiyo.

