Nahodha wa zamani wa klabu ya Real Madrid Sergio Ramos ruksa kurejea kuitumikia timu ya taifa ya Hispania ambayo hajaitumikia kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja sasa.
Kocha mpya wa timu ya taifa ya Hispania Luis de la Fuente ameeleza Ramos anaruhisiwa kuendelea kuitumikia timu hiyo ambayo amekua akiitumikia kwa muda mrefu na kushinda nayo mataji yote makubwa, Kocha Luis de la Fuente ni wazi amefungua milango upya kwa gwiji huyo.
Beki huyo anayekipiga katika klabu ya PSG kwasasa alitemwa kwenye michuano ya mataifa barani ulaya maarufu kama Euro mwaka 2021, Lakini pia alitemwa kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Qatar mwaka 2022 na kocha aliyepita ndani ya timu hiyo Luis Enrique.
Sergio Ramos mwenye umri wa miaka 37 kwasasa bado anaoneakana kua na nguvu ya kupambana kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania, Kutokana na hali hiyo ni jambo ambalo lilikua likiwashangaza mashabiki wengi wa Hispania kuona beki huyo anaachwa kwenye timu hiyo.
Mpaka sasa Luis de la Fuente amewasha taa ya kijani kwa Ramos kurejea kwenye timu ya taifa ya Hispania, Na hii inakua rahisi kwani licha ya gwiji huyo kutemwa mara mbili kwenye mashindano makubwa lakini hakuweza kutangaza kustaafu kulitumikia taifa hilo.

